Msanii lady jaydee yupo katika huzuni baada ya kuondokewa na dada yake kipenzi.
Hatua hii imemfanya msanii mwenzake ambaye pia ni swahiba wake aitwaye proffesor jay kuungana na naye katika msiba huo.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa face book msanii huyu amepost picha inayomuonesha akiwa katika msiba huo.
Pamoja na picha hiyo msanii huyu ameambatanisha  maelezo yanayoashiria kutoa pole kwa rafiki yake wa karibu msanii lady jaydee kwa kumpoteza dada yake.
"Msibani nyumbani kwa kina @LadyJayDee ambaye amefiwa na dada yake aitwae Lucy tangu juzi na mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kwenda Mkoani MARA Kwa mazishi. ... pole sana JIDE, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema PEPONI. .AMEN!!" liandika Proff
Tunapenda kutoa pole kwa msiba huo na Mungu ailaze roho ya marehemu peponi Aamin!!!!
 

 
Axact

Post A Comment: