Taarifa kutoka katika mtandao wa Perez Hilton wa nchini Marekani zinasema ugomvi wa Jay z na shemeji yake ulitokana
na ubishani uliokuwa ukiendelea baina yao.Habari zinasema ubishani huo ulitokana na shemeji yake huyo aitwaye Solange kumzuia Jayz asiende katika party ya Rihana na kuwa aende nyumbani ambapo hakuishia hapo aliamua kumtaarifu na dada yake kitu ambacho Jayz hakukubali na kutoa maneno yaliyoonesha kumkera Solange baada ya kumuita kuwa sio mama bora na anapenda kujirusha na ndipo Solange akaamua kumshushia kisago, wakati huo dada yake Beyoce akiwatazama. Hivi karibuni kulitokea tukio la ugomvi na la kushangaza lililowahusisha Jay Z na shemeji yake Solange katika lift ya hotel huko New york Marekani wakitoka katika after party ya met gala.


Axact

Post A Comment: