Kufuatia kuwa gumzo kwa baadhi ya watu hapa nchini na kuhoji juu ya mali alizo nazo msanii wa fialmu hapa nchini Irene Uwoya,ameamua kuvunja ukimya na kuzungumza
namna alivyozipata. katika mahojiano na mtandao wa Bongo5 msanii huyo alisema mali hizo zinatokana na sanaa ya filamu pamoja na shughuli nyingine binafsi. msanii huyo alieleza kuwa watu wanashindwa kuamin kama sanaa inaweza kulipa kiasi hicho na kuwa watu wa aina hiyo wana ufinyu tu wa akili. Aliongeza kuwa mara nyingi yeye hapendi kuweka vitu hadharani kama wengine ambao wakipata vitu wanatangaza na kuwa hupenda zaidi kufanya vitu kama yeye.
Post A Comment: