Msanii wa muziki kutoka jijini Mwanza Tanzania na mshindi wa tuzo mbili za Ktma anayefahamika kwa jina la Fid Q amesema kinachomkwamisha kufunga ndoa ni mtoto aliye
naye. Akizungumza na Global tv msanii huyo alisema anatarajia kuoa hivi karibuni lakini kinachompa mawazo ni mwanae aliyezaa na mwanamke mwingine tofauti na huyo anayetaka kumuoa.Akizungumzia uhusiano wake na salama msanii huyo alisema uhusiano wao ni wa kawaida na sio wa kimapenzi kama ilivyovuma kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. Alieleza zaidi kuwa mbali na watanzania wengi kujua hivyo ilifika hatua mpaka mama mzazi wa Salama kuamini kuhisi walikuwa katika uhusiano kutokana na ukaribu waliokuwa nao.



Axact

Post A Comment: