Msanii wa muziki
kutoka Kenya Avril Nyambura amesema pesa haikumfanya akubali kuwa na mchumba
mfanyabiashara tajiri wa Afrika kusini na badala yake ni mapenzi tu aliyo nayo.
Msanii huyu ametoa kauli hii kufuati uvumi uliosambaa nchini
humo kuwa ameamua kuwa na huyo mchumba wake kwa sababu ya utajiri alio nao
mfanya biashara huyo.
Akinukuliwa msanii huyu amesema "tumefahamiana muda
mrefu kama ni kuhusu pesa ningekuwa naendesha
Range Rover mwaka huu na nisingekuwa naishi south B.He is amazing na sijali
kile watu wasemacho"
Hivi sasa imedaiwa kuwa msanii huyo pamoja na mchumba wake
wako mjini Mombasa
kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Chrismas na wakijiandaa kuelekea Afrika
kusini kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya.
Hata hivyo imeripotiwa kuwa ndoa ya watu hawa haitofanyika
hivi karibuni kutokana na kutofautiana tamaduni na mila na hivyo kuna utaratibu
wataufanya.
Post A Comment: