Muanzilishi na mmiliki wa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen maarufu kama madam Rita amesema alipata mtihani mkubwa baada ya kupata ujauzito akiwa katika umri mdogo.

Kupitia ukurasa wake wa face book mama huyu amesema alipata wakati mgumu hasa ikizingatiwa kuwa jamii inayotuzunguka huona ajabu binti mwenye umri mdogo kupata ujauzito
Hata hvyo ameeleza kuwa pamoja na kukabiliana na changamoto hiyo bado alikabiliana nayo na hatimaye kufika hapo alipo hivi sasa na kuwashauri wasichana waliokumbwa na hali hiyo kutokata tamaa na kufanya juhudi ili kujikwamua.


"Jambo mmoja msilofahamu kuhusu mimi....

Nilipata ujauzito nikiwa na umri mdogo sana. Kwa jamii yetu inayotuzunguka, ukizaa katika umri mdogo, watu huwa wanakunyanyapaa, hukuona haufai kuwa katika jamii na hata kukuhukumu. Kwa umri ule niliona ni kama hamna tena maisha kwangu lakini sikukata tamaa na leo hii ujasiri wangu na kitu kinachonipa msukumo wa maisha hadi kufika hapa nilipo ni hicho kilichonikuta nikiwa na umri mdogo.

"Kukataa tamaa isiwe ndio chaguo lako la kwanza"
Axact

Post A Comment: