Msanii wa muziki wa RnB nchini tanzania ameelezea kisa kilichowahi kumtokea baada ya kupeleka baba feki shuleni ili kujinusuru na msala aliokuwa nao.

Akizungumza na Bongo20 msanii huyu amesema kuna msala uliwahi kumtokea kipindi anasoma ambapo alitakiwa kumepeka baba yake mzazi shuleni ili kufahamishwa utukutu anaoufanya mwananae.
Kwa mujibu wa
msanii huyu aliamua kuingia mtaani na kumchukua dereva tax ambaye alimuahidi kumpa shilingi elfu kumi endapo atamsaidia msala huo kwa kujifanya ni baba wa msanii huyu..
Kufuatia hali hiyo dereva huyo wa tex alikubali na kuongozana hadi shuleni ili apate buku te kwa kmsaidia ben pol.
Tofauti na matarajio yao mambo yalibadilika ambapo yule dereva baada ya kushtukiwa alishindwa kusema yeye ni baba wa nani kutokana na kutojua jina la Ben pol sababu Ben hakuwa amemuambia jina lake.
Ben pol akaendelea kufunguka zaidi kuwa jamaa alishindwa kujibu mbele ya walimu waliokuwepo katika ofisi ya yao.
Kufuatia hali hiyo mambo msala ukawa mkubwa zaidi kwa Ben pol ambaye alitandikwa viboko na kuambiwa akamlete mzazi wake halisi wakati yule feki akiondoka bila kufanikisha mipango yao.
Axact

Post A Comment: