Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Belle9 amesema kinachowasumbua wasnii wengi wa hapa nchini kutotambulika kimataifa ni kutokuwepo kwa connection nzuri baina yao na watu wa media katika nchi mbalimbali.
Akizungumza
na bongo20 msanii huyu amesema wasanii wa tanzania wengi wana uwezo mkubwa na wanafanya vizuri ila kinachowakwamisha ni namna ya kusambaza kazi zao kimataifa.
Ameeleza wapo baadhi ambao wameweza kufanya hivyo lakini kuna wengi ambao wanakosa namna ya kufikisha kazi zao kimataifa.
Akizungumzia mipango yake msanii huyu amesema anataka kuufikisha muziki wake mbali na tayari kuna baadhi ya wasanii wa nje ambao amekwisha anza mazungumzo nao akiwamo Wayre toka Kenya ambaye anatarajia kufanya naye kazi.
"Tayari nimeshafanya mazungumzo na Wyre na kuna kazi tutaifanya pia nimeshaanza mazungumzo na wasanii wengine wa nje ili nifanye nao kazi" alisema Belle.
Axact

Post A Comment: