Msichana mrembo aishie Uingereza, aliyetajwa kwa jina la Sunshine Haye, amejitokeza na kudai kuwa na ujauzito wa mkali wa ‘Skelewu’, Davido na kwamba anatarajia watoto mapacha.
Kwa mujibu wa Naijaxclusive mrembo huyo ambaye
anatokea Caribbean mwenye asili ya Jamaica pia amedai kuwa Davido alimpa ujauzito huo mwaka jana (2013) wakati alipokuwa kwenye ziara yake nchini Uingereza.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 23, amedai kuwa hivi sasa ujauzito huo umefikisha miezi kati ya minne hadi mitano na kwa mujibu wa tweets zake alizoandika mwaka jana anatarajia watoto mapacha. “Twins!! I think I’m gonna pass out.” Ni moja kati ya tweets za mrembo huyo.
Hata hivyo, watu wa karibu wa Davido walipozungumza na mtandao huo walikanusha taarifa hizo na kudai kuwa hawafahamu chochote kuhusu hilo.
Lakini camp ya mrembo huyo imesisitiza kuwa taarifa hizo ni za ukweli na kwamba watakuwa tayari kutoa vielelezo kuthibisha hilo.
Hii si mara ya kwanza kwa msichana kujitokeza na kudai kuwa na ujauzito wa Davido, July mwaka jana msichana mmoja Kenya alijitokeza na kuwaambia waandishi wa habari kuwa alikuwa na ujauzito wa Davido, lakini mwisho wa siku iligundulika kuwa taarifa hizo hazikuwa na ukweli wowote.
Post A Comment: