Msanii Sajna kutoka mkoani Mwanza Nchini Tanzani ambaye amewahi kutamba na ngoma kibao kama Sitaki kuumizwa na Iveta amefunguka ukweli uliojificha moyoni mwake kwa muda mrefu.
Msanii huyu alisema aliamua
kuandika wimbo wa samahani ambao una stori ya kweli ambayo imemtokea yeye mwenyewe.Akizungumza na mwandishi wetu msanii huyu amesema alikuwa na mpenzi ambaye walipendana lakini baadaye penzi lao likageuka shubiri baada ya wachonganishi kuingilia.
Msanii huyu alieleza kuwa kuna siku alikwenda kufanya show katika wilaya moja mkoani Mwanza na huko akakutana na binti mmoja aliyedai kumfahamu Sajna pamoja na mpenzi wake huyo.
Msanii huyu akafunguka zaidi kuwa alizungumza kidogo na binti yule na akagundua ni kweli alikuwa akiwafahamu na kama haitoshi alikuwa na urafiki na mpenzi wake huyo.
siku chache baadaye msanii huyu alipokea ujumbe ktuka kwa mpenzi wake uliyemtaka aachane naye kwa madai ya kumtongoza msichana aliyekutana naye kwenye show.
Msanii huyu alieleza kuwa hakukuwa na ukweli wowote juu ya madai hayo na kuwa kuna kitu kilipangwa ili kuwagombanisha.
"niliamua kufunga safari hadi nyumbani kwao na kumkuta mama yake mzazi ambaye aliniambia nimuache kwanza mwananaye atuli nna hasira zikiisha huenda akarudi na kuendelea na uhusiano".alisema Sajna
Hata hivyo hali hii haikubadilika na badala yake ameendelea na msimamo wake kitu ambacho kimenifanya kuandika wimbo wa samahani ili kueleza hisia zangu lakini pia kumuoba anisamehe kwa yote na tuendelee na maisha".Aliongeza msanii huyu.
Axact

Post A Comment: