Msanii Ney wa Mitego amewafungukia wasanii wanaowanaorudia nyimbo za wenzao kwa kuwadiss wasanii walioimba nyimbo original  

Kupitia ukurasa wake wa face book msanii huyu amesema kuna wasanii ambao wamekuwa wakisubiri wenzao watoe nyimbo na kisha wao kuzirudia kwa kutumia melody na beat kuwa diss wenzao ambao wametoa nyibmo original.
soma alichikiandika hapo chini 

"SOMA HII UJIFUNZE KITU..

Wasanii Bongo hatuangalii tunachokifanya na kukitilia mkazo wengi wao tunawaza flan afanye au akifanya hivi nimdis huko kutafuta kick sasa maana imekuwa inatokea mara kwa mara msanii flani anatoa ngoma mwingine anatumia aidha beat au sauti na kubadili. Msanii flani amepiga picha na flani anaona au ametoa collabo na msanii wa nje anaamua kumdis kutokana na kuona kwamba hawezi kufikia hizo level..!!!

Wa Mitego huwa anatoa dis kwenye Ngoma zake basi na wewe unatafuta njia yakuweza kumdis ili uonekane mwamba Ahhaah..

Usiku mwema Wadau nimefikilia Mengi kuandika huu ujumbe.

Mniache nile ujana aisee..
#Nakula_Ujana
Axact

Post A Comment: