Mzee Omary Dude - Enzi za uhali wake.
 Msanii wa kundi la vichekesho jijini Mwanza Futuhi aliyekuwa akifahamika kwa jina la mzee Dude amefariki dunia hapo jana majira ya jioni katika hospital ya Bugando alikokuwa amelazwa.

Habari zaidi zinasema msanii huyu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo ambayo yalimpelekea kulazwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupata matibabu hata hivyo juhudi za madaktari kuokoa uhai wake zilishindikana na na ndipo siku ya jana majira ya saa kumi jioni akaiaga dunia.
habari zaidi kuhusiana na kinachoendelea tutaendelea kukujuza kadiri tutakavyopata taarifa.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema
Axact

Post A Comment: