Wastara
Msanii wa kike wa filamu hapa nchini aitwaye Wastara Juma amesema amekuwa akikabiliwa na changamoto ya kuandikwa vibaya katika baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.
Habari zaidi zinasema msanii huyu ameeleza kuwa kuna vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiandika habari za ungo juu yake kitu ambacho kinamfanya asijisikie vizuri.

Wastara ameeleza vyombo hivyo vimekuwa vikimfuatilia tangu kufariki kwa marehemu mume wake aliyekuwa akitwa Sajuki ambapo wamekuwa wakiripoti kuwa anataka kuolewa kitu ambacho amedai si cha kweli.

"Nina changamoto nyingi sana,unajua siku zote kama mtu ukitaka kuheshimiwa basi heshima ndio msingi wa maisha,lakini tangu mume wangu afariki (Sajuki)kumekuwa na maneno mengi sana kwenye magazeti,mara nimeolewa sijui nimevishwa pete na ukija kuangalia mtu aliyeandikia hiyo habari unamjua na ukimpigia simu anaanza kukukwepa. Kama habari za kuolewa siwezi kwanza kutangaza,  naomba waandishi waandike habari za uhakika ili ujumbe ufike mzuri kwa wananchi wanaotutazama sisi Wasanii." Amesema Wastara.

Kauli kama hii imekwisha tolewa na baadhi ya wasanii wakike hapa nchini ambao walidai kutotendewa haki na vvyombo vya habari akiwamo muimbaji Shilole pamoja na baby Madaha.
Axact

Post A Comment: