Siku chache baada ya kuibuka na ushindi mkubwa katika tuzo za umahiri wa uandishi wa habari nchini(Ejat) na kupokea maombi ya watu waengi wakitamani kuisikia katka mikoa ya mbali na Mwanza kama Dar, Morogoro n.k, Afisa miradi wa shirika linaloiendesha Afya radio Bi Jane Benedict Alisema wapo katika
mpango wa kuongeza masafa ili kuwafikia watu wengi zaidi.Ameeleza mipango hiyo imekwisha kuanza na katika hatua ya kwanza watanaza na mikoa yote ya kanda ya ziwa.Akizungumzia ushindi wa tuzo kumi n moja ilioupata Afya radio kupitia wafanyakazi wake amesema ni ishara kuwa wanawafanyakazi wazuri, wachapakazi na sio wapenda sifa kama ilivyo kwa wengine. Afaya radio ilichukua tuzo kumi na moja ambapo Idi juma muandishi wa redio hiyo akichukua tuzo nne ikiwemo ya mshindi wa jumla.Tuzo nyingine alizochukua ni pamoja tuzo ya habari za walemavu, habari za mazingira, habari na habari za kilimo.Wengine waliochukua tuzo ni pamoja na Clara Patrick( Habari za afya na kundi la wazi),Secilia Ndabigeze(Habari za Sayansi na teknolojia),Penina Zakaria(habari za Ukimwi), Rejina Kulindwa(habari za Afya ya uzazi kwa vijana),Noel Thompson(Habari za elimu) na Harith Jaha (Habari za uchumi na biashara).
Washindi wengine waliochukua nafasi ya pili ni pamoja na Jackson Mwafulango(Michezo na burudani),Charles Urio (habari za walemavu),Khamis Abdallah(habari za walemavu) Curthbet Japhet(habari za afya ya uzazi kwa vijana),Noel Thompson(utawala bora),Penina Zakaria( jinsia),Secilia Ndabigeze (Malaria) na Harith Jaha(Elimu).Tazama hapo chini pichaza tukio la utoaji wa tuzo hizo kwa waandishi wa habari zilizofanyika tarehe kumi na nne mwezi wa tatu mwaka huu.
Kushoto ni Jackson Kweka, katikati ni Iddi Juma na kulia ni Harith Jaha

Iddi Juma akikabidhiwa tuzo ya mshindi wa jumla
Noel Thompson akipokea tuzo ya habari za elimu


Clara Patric akipokea tuzo ya kundi la wazi



Clara Ptric akipokea tuzo ya habari za Afya


Secilia Ndabigeze akipokea tuzo ya habari za Sayansi na Teknolojia
Secilia Ndabigeze akichukua zawadi ya mshindi wa pili Malaria
Penia zakaria akipokea tuzo ya habari za Ukimwi
Penina Zakaria akipokea zawadi ya mshindi wa pili habari za jinsia
Harith Jaha akipokea tuzo ya habari za uchumi na biashara
Harith Jaha akipokea zawadi ya mshindi wa pili habari za elimu
Rejina Kulindwa akipokea tuzo ya habari za afya ya uzazi

Axact

Post A Comment: