Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la BBC watafiti kutoka Ungereza na Uholanzi wamebaini kuwa dawa za meno zinazotumika kila siku zina kemikali zinazoathiri uwezo wa mbegu za mwanaume kumpa ujauzito mwanamke.Katika taarifa hizo zilizoandikwa katika
jarida la Embo zinasema katika utengenezaji wa dawa hizo kuna kemikali inayojulikana kama Triclosan kemikali inayoharibu kabisa uwezo wa mbegu za kiume kufikia yai la mwanamke na kutunga mimba.Mbali na dawa za meno pia mafuta ya kujipaka na sabuni za kuogea navyo vimetajwa kuwa na kemikali hizo.Habari zinasema kati ya wanaume sita waliooa nchini Uingereza mmoja kati yao anasumbuliwa na tatizo hilo.
Post A Comment: