Mke wa marehem Dr. Gilbert Buberwa akifarijiwa
Wizara ya Afya na ustawi wa jamii imewataka wananchi kuwa makini  na kutumia vyandarua vyenye dawa pindi walalapo mchana ili kujinusuru na ugonjwa wa dengue uliolipuka hivi karibuni jijini Dar es salam. Akizungumza bungeni mjini Dodoma hapo jana 
naibu waziri wa wizara hiyo Dk. Kebwe Steven alisema mbu hao aina ya Aedes Egyptae wanang'ata mchana na kuwa hupendelea kukaa kwenye maji masafi hivyo ni vyema kioa mwananchi akawa makini kwa kuondoa maji yote yaliyo wazi sambamna na kutumia dawa za kuuwia mbu katika vyandarua.Ameeleza hadi hivimsasa bado hakujapatikana tiba wala chanjo ya ugonjwa huo na hivyo njia pekee ya kupambana na ugonjwa huo ni kuzuia uchafu pia kuvaa nguo ndefu.Hadi hivi hivi sasa tayari kumeripotiwa watu kadhaa kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo akiwemo daktari bingwa wa hospitali ya Temeke Dr. Gilbert Buberwa.

Axact

Post A Comment: