Katika hali ya kushangaza msichana mmoja jijini London anayefahamika kwa jina la Claire leeson mwenye umri wa miaka 24 ameamua kutumia kiasi cha $30,000 (Tsh 49,755000) za kibongo kwa ajili ya kutengeneza sura ili ifanane ya Kim Kardashian.
Akizungumza na chombo cha habari cha This Morning Claire ameeleza aliamua kufanya hivyo kwa sababu alipokuwa shuleni wenzake walikuwa wanamcheka na kuuita ‘mbaya’ kuliko kitu chochote kilicho hai.
“Nilikuwa naambiwa kila siku mimi ndiye mbaya kuliko kitu chochote kilicho hai na kwamba inabidi nijiue. Nilipoacha shule marafiki zangu waliniambia kuwa ninavitu ambavyo vinafanana na Kim Kardashian.” Amesema Claire.
Ameeleza kuwa baada ya kuambiwa hivyo na marafiki zake aliamua kuanza kufuatilia kwa ukaribu kauli hiyo kwa kujichunguza yeye na Kim na ndipo akagundua kuwa kweli kuna vitu ambavyo wanafanana na Kim Kardashian na ndipo alipoamua kufanya upasuaji ili afanane naye kabisa.
Paoja na
msichana huyo kulaimika kuingia katika madeni amesema anaona alichokifanya
kinathamani zaidi ya fedha aliyotoa.
Post A Comment: