Wafanyakazi mia nne kati ya elfu
moja na mia tano wa shirika la mtandao
wa simu wa TTCL huenda wakajikuta katika wakati mgumu baada ya kuwa hatarini
kupoteza kazi zao.
Hatua hii inaelezwa ni kutokana
wafanyakazi hao kutokuwa na majukumu yanayoeleweka hali inayowafanya kufika
ofisini na kukaa tu kuanzia asubuhi hadi jioni hali ya kuwa wanalipwa mishahara
yenye kiwango kikubwa kuanzia laki nane.
Ofisa mtendaji mkuu wa shirika hilo Dr. Kamugisha Kazaura alisema maaalizi
ya kuwafuta kazi watu hao yataanza mwezi aprili mwaka huu kupitia ukaguzi
maalumu wa rasilimali watu .
Post A Comment: