Serikali imeombwa kutengeneza
utaratibu au kupiga marufuku watoto wanaoingia mitaani kusherehekea sikukuu
bila usimamizi wowote na kusababisha ajali kwa watoto hao.
Imekuwa ni awaida katika kila siku
kuu kuwaona watoto wakisherehekea katika maeneo mbalimbali ya miji ikiwemo jiji
la mwanza katika mzunguko wa samaki na maeneo mengine.
Hata hivyo badhi ya watoto hao
wanaonekana kutokuwa na usimamizi wa kutosha hali inayowaweka katika hatari ya
kukumbwa na madhara mbalimbali ikiwemo ajali jambo linalowafanya wakazi wa jiji
la mwanza kuomba hata kuzuiwa kwa utaratibu huo.
Naye afisa wa polisi kitengo cha
usalama barabarani wilaya ya nyamagana mkoani mwanza koplo jeremia makolomu anasema
wazazi wanatakiwa kuongeza umakini zaidi kwa kuwa huwapa kazi ya ziada katika
kuwasaidia watoto hao.
Post A Comment: