Mamlaka ya maji
safi na usafi wa mazingira katika jiji la mwanza
imetakiwa kuboresha huduma zake ili kuondoa malalamiko ya kukatika kwa maji
mara kwa mara.
Mji wa mwanza ni
moja kati ya miji iliyopata bahati ya kuzungukwa na ziwa victoria ,ziwa
linalotajwa kufika hata katika nchi jirani kama kenya na uganda.
Hata hivyo baadhi
ya wakazi wa mji huu wanasema licha ya kuzungukwa na ziwa hilo bado haijawa
tiba ya kuwaondolea kero ya uksefu wa maji na kuiomba mamlka ya maji safi
kuweka nguvu zaidi katika kutatua kero za maji.
Kaimu afisa uhusiano wa mamlaka hiyo jijini Mwanza Bw. Oscar Tuwakazi alisema wapo katika mpango wa kuboresha huduma zao na kuwafikia watu wengi
zaidi.
“tayari
tumeshawasiliana na Tanesco na wametushauri tongeze vituo vya kusambaza maji na
wao watatuunganishia umeme ambao hata kama kuna mgao hautakkatika katika vituo
hivyo” alisema Tuwakazi.
Post A Comment: