watoto wa mitaani wakiomba fedha za kuendesha maisha yao kwa wasamariawema |
Ongezeko la watoto wa mitaani
limeelezwa kuchangiwa na tabia za badhi
ya wazazi kjiingiza katika uhusiano na waume au wake za watu hali inayoleta
ugumu katika utoaji huduma kwa mtoto ambaye anazaliwa kutokana na uhusiano huo.
Afisa ustawi wa halmashauri ya jiji
la mwanza Edith Ngowi amesema wamekuwa wakipokea kesi nyingi za malalamiko ya
kutlekezwa kwa watoto hasa wale ambao hawapo katika mahusiano rasmi.
Nao baadhi ya wakazi wa jiji la
mwanza wanasema kuna haj kwa wanaume na wanawake kutafakari kabla ya kujiingiza
katika uhusiano na watu wasio na mipango nao.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi
ya ustawi wa jamii katika halmashauri ya jiji la mwanza kesi za utelekezaji
ujauzito huripotiwa tatu hadi nne kwa siku.
Post A Comment: