Msanii Kala jere miah kutoka jijini Mwanza Tanzania anayetamba na ngoma ya walewale amesema anafuraha kubwa kupata nafasi ya kufanya kazi na msanii
ambaye alikuwa akimsikia tu katika vyombo vya habari na na kumzungumzia geto na washikaji zake .
Msanii huyu amesema ni muda mrefu uliopita alikuwa akisikia jina la Juma nature katika vyombo mbalimbali vya habari na pia katika nyimbo mbalimbali wakati huo yeye akiwa hana matumaini kama kuna siku atapata nafasi ya kufayna naye kazi lakini Mungu si Athumani hatimaye amefanikiwa kumpata na kufanya naye kazi mbili ambazo kila mmoja amemshirikisha mwenzake.
Hata hivyo bado hajaweka wazi majina ya nyimbo hizo lakini alichokisema ni kuwa ataachia hivi karibuni ngoma mpya ambayo amemshirikisha Juma nature.
Axact

Post A Comment: