Msanii wa muziki hapa nchini Ney wa mitego amesema kabla hajawa msanii aliwahi kuchukua pesa ya mama yake bila idhini na kuingia katika mazingaombwe ili
pesa ile iongezeke na kufika elfu kumi.
Akizungumza na Bongo20 msanii huyu amesema kuna kipindi aliagizwa na bi mkubwa wake dukani na wakati yupo njiani aliona kuna watu waliokuwa wanafanya mazingaombwe ambapo waliokuwa wakicheza walionekana pesa wanazotoa kuongezeka baada ya kufanyiwa mazingaombwe ndipo alipoamua kurudi nyumbani na kuchukua ela ya mama yake shilingi elfu moja na kujiingiza katika mazinga ombwe hayo ambapo alipewa bahasha iliyopakwa majivu na kuambiwa aende nayo nyumbani bila kuifunua kisha akifika aifunike mahali kwa muda kisha aifungue atakuta ile pesa imeongezeka na kuwa elfu kumi.
Msanii huyu amesema baada ya kukaa muda fulani aliifungua na hakukuta kitu ndipo alipogundua kuwa alikuwa ametapeliwa.
Aliamua kumueleza mama yake ukweli kkwa kuwa haikuwa tabia yake kuiba na aliichukua ile fedha akiamini angeirudisha, hata hivyo mama yake huyo alimumind kidogo na kisha kumcheka kwa kutapeliwa hali ya kuwa amekulia mjini.
Je vipi kluhusu wewe uliwahi kuwaamini wacheza mazingaombwe?.
Post A Comment: