Ni swali ambalo mashabiki wengi wa muziki wanajiuliza juu ya msanii Soulja boy kutoka Chicago Marekani ambaye ametoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii wa twitter kuwa ataingia jela mwishoni mwa wiki hii.
Kupitia ukurasa wake msanii huyu ameandika maelezo yanayoonesha kuwa ataingia jela kitu ambacho watu wengi hawakufikiria.
“5 more days until I go to jail. Appreciate everyone who was there for me while I needed y'all.” Alitweet Souja Boy bila kutoa ufafanuzi zaidi.
Hata hivyo kuna taarifa kutoka katika mtandao wa Tmz zinazosema kuwa msanii huyu hivi karibuni alishitakiwa kwa kosa la kuwa na bunduki na kuvuka bila kusimama katika eneo alilopaswa kusimama huko Los Angeles.
Post A Comment: