Baada ya kiongozi wa kampuni ya Mtanashati Entertainment Ostaz juma na musoma kukaririwa katika vyombo vya habari kuwa ameamua kuachana na msanii toka Mwanza
Pnc,msanii huyu ameendelea kusisitiza kuwa yeye ni mtu mwenye nidhamu na sivyo kama ilivyosemwa na Ostaz.
Msanii huyu ameelza kinachotokea hivi sasa bado hajaelewa lakini kwa kuwa Ostaz ameamua kuachana nanye yeye ameridhia na kuwa ataendelea na shughuli zake za muziki.
Hivi karibuni kumekuwa na mvutano baina ya Pnc na bosi wake wa zamani Ostaz Juma ambapo bosi wake huyo alimtuhumu Pnc kufanya show bila kutoa taarifa.
Msanii huyu Pnc sasa anakuwa ni msanii mwingine aliyeachana na kampuni hiyo ambapo msanii mwingine aliyetoka ni Dogo Janja
Post A Comment: