Msanii Lady Jaydee kutoka Tanzania amteoa nafasi kwa mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kuhudhuria katika party ya kuzindua video ya wimbo
wake mpya wa " Historia"
Msanii huyu ameweka wazi jambo hilo kupitia ukurasa wake wa face book ambapo amesema kuna swali atauliza na kisha watu ishirini wa kwanza watakaopatia watapata nafasi ya kuwa wakwanza kuiona video hiyo ikiwa ni pamoja na kupata mualiko wa kuhudhuria party hiyo.
Lady Jaydee
Video ya Historia iko tayari na itatoka Jumamosi ya tar 8 february 2014 kwenye party maalum ya kuitambulisha, na kutoka humu facebook nitaalika watu 20 wa kuja kuiangalia kwa mara ya kwanza kabla haijaruka kwenye TV zote.. Swali litakuja na 20 wa mwanzo watakaopatia nitajumuika nao. Usicheze mbali.
Hatua hii ya msanii huyu imeonesha kufurahiwa na mashabiki wake na kuwaletea shauku ya kutaka kufahamu ni swali gani atauliza ili wapate nafasi hiyo.
Axact

Post A Comment: