Siku chache baada ya kiongozi wa kundi la muziki nchini Tanzania mtanashati Enter tainment Ostaz Juma na Muosoma kumshutumu msanii wake Pnc kuwa amekuwa na kiburi na kuwa hawezi kumsaidia msanii wa namna hiyo Pnc aibuka na kujibu tuhuma hizo.
Akizungumza na
Bongo20 msanii huyu Pnc amesema hakuna kosa ambalo amelifanya na ameshangazwa na hatua ya bosi wake kumsema vibaya katika vyombo vya habari.
Msanii huyu ameeleza awali hakuwa anajua nini kinaendelea kutokana na ukimya aliouonesha bosi wao huyo hali ambayo ilimfanya awe njia panda na asijue muelekeo wake.
Siku chache baadaye alipata taarifa kuwa bosi wao huyo anamsema vibaya katika vyombo vya habari.
Msanii huyo ameeleza kuwa yeye hajafanya kosa lolote na kama kuna kosa labda lilitokea kipindi cha nyuma na hata hivyo kama lipo alipaswa kumuambia mwenyewe wakajua cha kufanya na sio kuenda katika vyombo vya habari
Msanii huyu amesema anamtafuta bosi wake huyo ili kujua hatma yake
Hivi karibuni kumekuwa na mvutano kati ya Pnc na meneja wake ambapo meneja huyo amedai kuwa Pnc amebadilika na kuwa na kiburi kutokana na kpata umaarufu.
Msikilize hapa

Axact

Post A Comment: