Taarifa kutoka katika mtandao wa Tmz zinasema askari nchini marekani wanaitafuta video inayodaiwa kumuonesha msanii  Philip Seymour Hoffman aliyeripotiwa kupoteza maisha kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya aina ya Heroine.
Habari zinasema msanii huyu alirekodiwa na kamera ya kwenye mashine ya ATM mapema kabla hajafikwa na umauti.

Mtu mmoja aliyemuona msanii huyo akiwa eneo alilokuwa akitoa pesa ameeleza msanii huyo wa filamu alichukua kiasi kikubwa cha pesa na kisha kuzungumza na watu wawili wanaosadikiwa walikuwa ni wauzaji wa dawa za kulevya.
Polisi nchini humo wanatafuta video hiyo ili kupata ushaidi wa tukio hilo ikiwa na katika hatua za kukamilisha uchunguzi wa kifo chake.
Msanii huyu ameripotiwa kufariki dunia akiwa bafuni kwake kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha dawa za kulevya utumizi ambao umedaiwa ulikuwa umepita kiasi.
Axact

Post A Comment: