Akizungumza na Times FM website, Steve amesema lengo kubwa la kuandaa kipindi hicho ili kuelimisha Jamii, pia kuwakutanisha wasanii watakaokuwa wakizungumza na mashabiki wao
"Muda si mrefu watanzania kwa ujumla watakuwa wananiangalia kupitia channel za TV, lakini siwezi kusema ni channel gani, nitakuwa nafanya kitu kinaitwa ‘Steve Stand Up Comedy". Steve ameiambia tovuti ya Times Fm.
Ameongeza kuwa mbali na kuonesha kwenye channel za runinga, atakihamishia kwenye sehemu ambazo watu watakuwa wanaingia na kulipia kuona moja kwa moja kinachofanyika.
"Lakini kitakuwa na kiingilio sehemu fulani, kwa sababu nimeona watanzania wengi hawana sehemu maalum siku ya Jumapili zaidi ya kwenda Coco Beach,Leaders Club kwa hiyo naandaa kitu ambacho kinakuwa cha tofauti kabisa."
Amesema pia anaweza kuwa anawaalika wachekeshaji mbalimbali kutoka nje ya nchi ili waweze kuja Tanzania kuwaona na kuwaburudisha mashabiki wao.
Post A Comment: