Msanii lady Jaydee ametangaza kufunga shindano lake la kuwatafuta mashabiki ishirini watakao kuwa wa kwanza kutazama video yake mpya.
Kupitia ukurasa wake wa face book msanii huyu ameandika kuwa shindano lake la kutafuta watu ishirini watakao kuwa wa kwanza kuiona video yake mpya ya wimbo wa Historia limekwisha na atatangaza majina ya washindi leo saa kumi jioni.

Soma alivyoandika hapo chini
Lady Jaydee
“Shindano limefungwa, washindi wamepatikana na majina yao yatatajwa kuanzia saa 10:00 jioni na kuendelea, yani leo leo”.
Ukiona jina lako tafadhali inbox namba ya simu

Awali msanii huyu aliuliza swali kama ifuatavyo hapo chini

SWALI : Wimbo wa Distance umeimbwa kwa lugha ngapi na ulitoka mwaka gani?

ZINGATIA: Washiriki wasiwe wale waliokwisha shinda ticket za Valentine ili wengine wapya nao wapate nafasi
Twende Kazi.

Lengo la msanii huyu kufanya hivyo limetajwa kuwa ni katika kuwa karibu zaidi na mashabiki wake
Axact

Post A Comment: