Pamoja na juhudi za serikali na mashirika mbalimbali kufanya jitihada za kuwaelimisha wanaume juu ya faida za kutahiriwa na hasara za kutofanyiwa kitendo hicho hapa nchini bado kuna baadhi ya watu wanaoendelea kupinga kwa kigezo cha mila wakidai sio sawa kufanyiwa kitendo hicho.Kwa mujibu wa daktari kutoka hospitali ya mwananchi jijini Mwanza Dr.Wales Keto mwanaume ambaye hajatahiriwa yupo kwenye hatari ya zinaa na hata kansa kwa urahisi.Daktari huyo anaeleza Kansa hiyo hutokana na uchafukatikakati ya kichwa cha uume na ngozi ya mbeleya uume(govi)ambapo uchafu huo huwa na wadudu wanaoleta madhara si kwa manaume huyo tu bali pia kwa mwenzi wake ambapo anaweza kumsababishia kansa ya shingo ya kizazi kutokana na uchafu ule kuingia katika uke wa mwanamke wakati wa kujamiiana.Mbali na kansa pia magonjwa ya zinaa ni rahisi kumpata mtu ambaye hajatahiriwa na pia huwa ni rahisi kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Sikiliza na download sauti ya Dr. Keto akielezea madhara ya kutotahiriwa
Post A Comment: