Msanii kutoka jijini Mwanza Young Killer Msodoki amesema muziki wa sasa umetawaliwa na fedha na sio kipaji tena kama ilivyokuwa zamani.Msanii huyu amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa kutokana na hali inavyokwenda katika siku za usoni muziki huu utamilikiwa na wenye fedha tu na kuwaacha chipukizi wakisota kutafutafuta namna ya kutoka.
Aliongeza kuwa yeye binafsi alishawahi kusota sana kutafuta namna ya kutoka lakini ilikuwa ngumu licha ya kuwa alikuwa amezunguwa na watangazaji kutoka katika media tofauti.MMbali na msanii huyo kuzungumzia swala hilo pia kumekuwa kukisikika malalamiko kama hayo toka kwa wasanii wachanga wanaofanya muziki wao jijini Mwanza
Post A Comment: