|
Katikati ni Rais wa Vicoba Tanzania Bi Devotha Lukokora |
Wanachi jijini Mwanza wameshauriwa kujiunga na viundi vya ujasiriamali ili kupata mikopo kwa urahisi na kujikwamua kiuchumi.Mratibu wa Vikundi vya kujiinua kiuchumi (Vicoba) Mkoa wa Mwanza Bw. Kamara Almasi akizungumza na Afya radio mwanza alisema watu wengi wamekuwa wakihangaika na wimbi la umasikini kutokana na kutojua namna ya kujiajiri na kujiingizia kipato.Ameeleza kutokana na mfumo wa nchi ulivyo watu wanapaswakujiunga katika vikundi vya kuweka na kukopa fedha ili kupata mikopo kwa urahisi akitolea fano vikundi vha Vicoba. Aliongeza zaidi kuwa kujiungana Vicoba kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupata mtaji,vitendea kazi na pia elimu ya , uendesha biashara.Bw. Kamara alieleza kuwa ili kujikwamua kimaendeleo kunahitajika jitihada za dhati na hivyo wananchi wajiunge na Vikoba kwa kuwa kuna upatikanaji wa mikopo kwa urahisi kuliko Taasisi nyingine za Kifedha.
Post A Comment: