Wananchi wa mtaa wa miembeni b uliokuwa ukijulikana kama lidepu bugando jijini mwanza wanakabiliwa na kero mbalimbali zisizokuwa na kikomo kutokana na kukosa mwenyekiti wa kuongoza mtaa huo baada ya aliyechaguliwa kujiuzuru
Wananchi hao walisema hivi sasa hivi sasa wanategemea huruma ya mwenyekiti wa mtaa jiran kutatua kero zao ambapo naye wakati mwingine hushindwa kutokana na kuelemewa na shughuli za mtaa wake.
Mkazi
wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina moja la Boniventure alisema
kukosekana kwa mwenyekiti katika mtaa huo kunawafanya wananchi hao kukosa sehemu ya
kupeleka malalamiko yao na hivyo kero zao zikibaki bila ya kutatuliwa
Hivi
karibuni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa
tamisemi Agrey Mwanry akijibu swali
bungeni alisema hakutakuwepo na uchaguzi katika sehemu ambapo kiongozi wake
amejiuzulu badala yake kutafanyika uchaguzi kwa sehemu ambazo kiongozi aliye
kuwepo amefariki
Mwenyekiti
wa mtaa wa miembeni b alijiuzuru miezi minane tu baada ya kuchaguliwa
na kusababisha pengo katika mtaa huo ambalo limedumu kwa zaidi ya miaka mitatu
bila kiongozi hali inayosababisha wananchi wa mtaa huo kukosa mahali pa
kupeleka kero zao
Post A Comment: