|
Halmashuri
ya wilaya ya ilemela mkoani mwanza imesema ina imani na utaratibu watendaji na wenyeviti wa
mitaa wa kutunga sheria ndogo za usafi na kuwa utasaidia kupunguza kero ya
uchafuzi wa mazingira.Utungwaji wa sheriamhizo utatoa uhuru kwa uongzio wa mtaa kuwachukukia hatua wale wote watakao bainika kuchafua mazingira.
Kauli
hii imetolewa na mkuu wa wilaya ya ilemela Mkoani Mwanza Amina Masenza akizungumzia juu ya mrundikano wa taka
uliokithiri katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo na yale ya kutupia taka .Amesema uwepo wa sheria hizo utasaidia katika kupambana na uchafuzi wa mazingira katika wilaya hiyo
Aidha amesema uongozi wa halmashauri hiyo unakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi na hivyo kusababisha kurundikana kwa taka katika maeneo ya kukusanyia.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko ya uwepo wa mrundikano wa taka katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo likiwemo la soko la kirumba.
Post A Comment: