Wanafunzi wanne wilaya ya nyamagana mkoani mwanza wameshindwa kuripoti katka shule walizochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari baada ya kubainika kuwa a ujauzito.
Mkuu wa wilaya ya nyamagana baraka konisaga amesema baadhi ya wanafunzi hao wamebainika kuolewa na mwingine kujifungua huku uongozi wa halmashauri ya jiji la mwanza ukipanga kufuatilia hatma zao.
Afisa elimu sekondari jiji la mwanza japhet oswi anasema matumizi ya simu yanachangia kuendeleza wimbi la ujauzito.
Nao baadhi ya wakazi wa jiji la mwanza wanasema kuna umuhimu kwa wazazi kuwazuia watoto wao kutumia simu.
Baadi ya wasichana waliopata ujauzito shuleni wanasema ni muhimu kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao pia watoto wenyewe kutambua madhara ya vishawishi.
Axact

Post A Comment: